Thursday, 30 June 2016

UJASIRIAMALI TIMEEEEEEE!

NDUGU WALIMWENGU WENZANGU, HABARINI ZA SAA HIZI! NAAMINI NYOTE NI WAZIMA NA KWA WALE WENZETU WALIOPO MAHOSPITALINI TUWAOMBEE HIMA MANANI AWAPONYE HARAKA WARUDI DIMBANI TUENDELEE KUJUMUIKA SOTE KATIKA KINYANG'ANYIRO HIKI CHA KUUPIGA VITA UMASIKINI.

SIKU YA LEO NAPENDA KUWAPATIA DARASA LA MUDA:

NAJUA UTASHANGAA KUSIKIA DARASA LA MUDA,
       LAKINI TAFADHALI KATAA KITINI NIKUPATIE HIZI BARAKA ZA KIUCHUMI NA ZA KIUJASIRIA MALI.


MAANA YA NENO MUDA:

MUDA NI KITU KINACHO KUJA NA KUONDOKA JAPO KINAJIRUDIA RUDIA KILA SIKU. MAISHA YAKO YOTE YAMEJIFICHA CHINI YA MUDA NA UKIWA MBUNIFU WA KUUCHEZA MCHEZO WA KUHESHIMU MUDA BASI UTAUFAIDI MUDA NA MATUNDA YAKE;

KUMBUKA MAISHA YAKO NI MUDA WAKO NA MUDA WAKO NI MAISHA YAKO!

JITAHIDI KILA SEKUNDE ISIKUPITE BURE BILA KUFANYA KITU CHANYE TIJA KATIKA MAISHA YAK, JAP ONI NGUMU LAKINI NAKUOMBA UJILAZIMISHE KWA HALI NA MALI KATIKA KUUJALI MUDA


       IMEANDALIWA NA MVUNGI KOMBO ABDALLAH

              MJASIRIAMALI NA MTUNZA MUDA KWA MAFANIKO YA MAISHA

Wednesday, 29 June 2016

MAHAKAMA KUU KANDA YA ARUSHA YA TENGUA USHINDI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA LONGIDO KWA TIKETI YA CHADEMA

Leo June 29 2016 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetengua matokeo ya ushindi yaliyompa Ubunge, Onesmo Nangole ‘CHADEMA’  jimbo la Longido kutokana na udanganyifu.
Akisikiliza kesi hiyo Jaji Sivangilwa Mwangesi amesema fomu zilizotumika kuandika matokeo ni fomu 21b za udiwani badala ya kutumia fomu 21c za ubunge hivyo uchaguzi utarudiwa.
Kesi hiyo ilifunguliwa mnamo June 29 2016 mahakama kuu Arusha na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ jimbo la Longido Dk. Steven Kiruswa.
Baada ya ushindi wa kesi hiyo dhidi ya Onesmo Nangole ‘CHADEMA’ Dk. Kiruswa ‘CCM’ amesema…..>>>’tunangojea wenzetu kama wana sababu ya kukata rufaa, wakate baada ya hapo tutaenda uwanjani kuanza upya….tulikuwa na madai mengi ya msingi lakini moja ni kuwepo kwa kasoro katika utaratibu waliotumia kuhesabu, kujumlisha na kutangaza matokeo ya uchaguzi

Tuesday, 28 June 2016

KUFURU YA DIAMOND KWA BILLION 9

Kumekuwepo na tetesi nyingi kuhusu utajiri wa Diamond umefikia kiasi gani. Hilo ni swali ambalo hajawahi kulijibu kwa uhakika zaidi ya kutoa tu hints na kuwaacha wanaouliza kubaki na majibu yao wenyewe vichwani.

Lakini kupitia kipindi maalum cha kituo cha runinga cha E!TV, E Vip kilichorushwa Jumapili ya June 26, tunaweza kusema walau kwa uhakika staa huyo ana utajiri mkubwa kiasi gani. Diamond ana utajiri wa dola milioni 4 za Kimarekani ambao kwa shilingi ya Tanzania ni zaidi ya bilioni 8.6.

Si kitu kinachoshangaza tena kwa Diamond kutokana na hatua aliyofikia akiwa msanii anayelipwa fedha nyingi zaidi Tanzania kwa sasa. Fedha zake nyingi zinatokana na show zake zisizokauka za ndani na nje ya nchi, mikataba ya ubalozi na matangazo kutoka makampuni kama Vodacom, Cocacola, DSTV na Red Gold. Hivi karibuni alipata deal jingine la kutangaza huduma ya taxi ya Uber.

Pia amekuwa akiingiza fedha nyingi kupitia biashara ya nyimbo zake hasa miito ya simu, malipo ya mirabaha kutoka nchi za jirani kama Kenya bila kusahau biashara za mtandaoni zikiwemo Youtube.

Uwekezaji wake kwenye label ya WCB ni kitu kingine kikubwa ambacho kitaanza kumuingizia fedha nyingi siku za usoni. Hadi sasa amesaini wasanii wanne wakiwemo Rich Mavoko, Raymond, Harmonize na dada yake Queen Darleen.

Lakini pia staa huyo anafahamika kwa kuwekeza zaidi fedha kwenye ardhi na nyumba huku akidaiwa kumiliki maeneo mengi jijini Dar es Salaam.